Pia aliunga mkono suala la DC huyo kumuita mtumishi mwenzao kuwa amepata shahada kwa kutumia nguo ya ndani na kesi ipo mahakamani huku akiwa na dharau, kiburi, kashfa na kufanya kazi kinyume cha taratibu.
“DC huyu akijua kuwa yeye ni kiongozi amekuwa na dharau na kudhalilisha viongozi wenzake kwa kuwatukana wale wote wanaofanya kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu na kukataa kutii maamuzi yake ambayo ni kinyume,” alisisitiza.
Kutokana na kumpa muda wa kuwasilisha vielelezo shahidi wa tatu, shauri hilo liliahirishwa mpaka kikao cha baraza kijacho ambapo vielelezo vitakuwa vimepatikana.
Wakati huo huo, baraza hilo lilisikiliza mashauri dhidi ya madiwani watano wakiwemo wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao wanadaiwa kutowasilisha tamko la mali na madeni kwa mujibu wa sheria.
Waliotuhumiwa ni Diwani wa Magomeni, Julian Bujugo (CCM) aliyekiri kutowasilisha tamko hilo mwaka 2012 kutokana na kuwa mbali na mkoa yaliyosababishwa na kufiwa na mke wake, Diwani wa Kata ya Kijitonyama, Uoleuole Juma (Chadema) ambaye kesi ya Uchaguzi bado iko mahakamani.
Wengine ni Diwani wa Kata ya Kunduchi, Janeth Rite (Chadema) aliyedai kupeleka fomu hizo, lakini akashangaa kuambiwa hazijafika, Diwani wa kata ya Sinza Renatus Pamba ambaye alisema amewasilisha tamko na nakala anazo, lakini shauri lake halikukamilika baada ya Mwenyekiti kubaini wanaapa bila kutumia vitabu vya dini.
Jaji Msumi alilalamika kutopelekwa kwa Biblia na Kurani kwa ajili ya kuapa na kusema viapo vyote havikuwa halali na kuahirisha mashauri yaliyobaki hadi leo.HABARILEO
0 comments:
Post a Comment