ASKOFU KILAINI, PROF TIBAIJUKA, CHENGE WALIJILAZIMISHA KUINGIA KATIKA UONGOZI, VIONGOZI WALIOCHOTA FEDHA ZA TEGETA ESCOW WAMEKOSA SIFA 10 ZA UKINAIFU.
Rais Kikwete akiwa na Mussa Ally Bwakila.
Na Mussa Ally Bwakila.
VITO KUMI VYA THAMANI:
1. Ukinaifu ni utajiri wa moyo, na utajiri wa moyo humfanya kiongozi kutohitajia visivyo halali yake.
2. Ukinaifu ni sifa inayomfanya Kiongozi aliyejipamba nayo kutarazaki kwa kadri ya kile kinachotosha hitajio lake.
3. Ukinaifu humfanya kiongozi kupanga maisha yake na ya jamii yake kwa kutumia akili timilifu.
4. Ukinaifu humzuia kiongozi kutoharibu shaksia yake na ufanisi wake wa uongozi.
5. Ukinaifu humfanya kiongozi kuacha tamaa ya kiwazimu na uroho wa kihayawani kwa kutofisidi mali ya umma.
6. Kutokinai kwa kiongozi, husababisha kuwa mtumwa wa tamaa na uchu wa mali zisizo halali yake.
7. Hakuna ugonjwa mbaya kwa kiongozi kama ule wa kutokinai, jambo ambalo humsukuma kujipamba kwa sifa ya tamaa ya kufuja dhamana na amana ya uongozi aliyopewa na umma aitunze.
8. Kutokinai hudhuru mwili na akili ya kiongozi; huipa taabu raha kwa kuitia karaha, na kuipa hofu furaha badala ya ujasiri.
9. Kutokinai kwa kiongozi huangamiza maisha na maendeleo ya jamii yake.
10. Kutokinai humsukuma kiongozi kuwa na tabia nyingine zote mbaya...
0 comments:
Post a Comment