Ujenzi barabara ya kulipia Dar- Chalinze waiva.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Steven Wasira.
KAMPUNI 12 zimejitokeza kuwania zabuni ya kujenga barabara mbadala kati ya Dar es Salaam hadi Chalinze kwa kiwango cha Expressway ambayo itakuwa ya kulipia.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Steven Wasira aliyasema hayo juzi bungeni wakati akichangia Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).
Bila ya kutaja majina ya kampuni hizo, Wasira alisema kampuni hizo 12 zimejitokeza kuwania zabuni ya ujenzi huo ambao utajengwa kwa utaratibu huo wa PPP.
Jana asubuhi, wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni, Naibu Waziri wa Ujenzi, Gerson Lwenge, alibainisha kuwa mojawapo ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kuimarisha barabara ya Morogoro, ni ujenzi wa Expressway kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze.
Alipowasilisha bungeni makadirio ya wizara kwa mwaka wa fedha 2014/15, Mei 23, mwaka huu, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alisema barabara hiyo mbadala itakuwa ya kulipia, na itajengwa kwa njia sita (lanes).
Dk Magufuli alisema barabara ya sasa itaendelea kutoa huduma kwa wale ambao hawako tayari kulipia. Barabara hiyo ina urefu wa kilometa 100.
Katika hatua nyingine, Serikali imesema itaajiri watumishi wa ardhi 220 ambao kipaumbele kitapewa maeneo ambayo hayana watumishi wengi wa sekta hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, alisema hayo jana bungeni akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ileje, Aliko Kiboba (CCM).
Kombani alisema watumishi hao watapelekwa katika maeneo yenye upungufu wa watumishi hao ikiwamo Wilaya ya Ileje, kama alivyoomba Mbunge Kibona.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kimataifa
/ TANZANIA KUJENGA BARABARA AMBAYO MADEREVA WATALAZIMIKA KULIPIA FEDHA ILI KUITUMIA, NI KUTOKA CHALINZE HADI DAR ES SALAAM
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment