BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WATANZANIA WAUNGANA PAMOJA KATIKA DUA YA KUMWOMBEA RAIS KIKWETE AFYA NJEMA BAADA YA UPASUAJI WA TEZI DUME NCHINI MAREKANI.


 
Rais Jakaya Kikwete
MAELFU wa wananchi mwishoni juzi waliungana katika ibada maalumu kumwombea afya njema Rais Jakaya Kikwete, aliyefanyiwa upasuaji wa tezi dume katika katika Hospitali ya Johns Hopkins Marekani hivi karibuni.


Katika ibada hiyo iliyoandaliwa na Kituo cha Huduna ya maombezi cha Good News for All Ministry na kufanyika Mapinga, wilayani Bagamoyo, waliojitokeza walimwombea afya njema Rais Kikwete na pia kumshukuru Mungu kwa uponyaji wake anaoendelea kuufanya kwa rais huyo.

Upande wa Serikali uliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi ambaye alitumia fursa hiyo kushukuru huduma ya kituo hicho, akisema kimeonesha ubinadamu wa kweli kwa kufanya ibada maalumu ya kumwombea Rais ambaye afya yake imeimarika na hata kutolewa wodini.

Alisema kutokana na kilichofanywa na huduma hiyo, viongozi na watu wa makanisa wanapaswa kuwa karibu na serikali kwa maombi siku zote, iwe za uzima au ugonjwa ili Mwenyezi Mungu aweze kuingilia kati na kufanya miujiza yake.

“Watu wa makanisa na imani tofauti ni vema kuiga mfano wa huduma hii kwa kutokuwa mbali na serikali na viongozi wake wakati wote kumuomba Mungu kwa uzima na ugonjwa, kwani wote tunaamini Mungu ndiye kila kitu kwa wanadamu,” alisema Kipozi.

Mwenyekiti wa Huduma hiyo, Askofu Charles Gadi alisema viongozi wa dini wana jukumu la kufanya maombi kwa kiongozi mkubwa wa nchi kwa nia ya kumuomba Mungu amponye na kurudi salama nchini.

“Baada ya Rais kurejea nchini tutafanya ibada maalumu ya kumshukuru Mungu kwa uponyaji wake, kwani tumemuomba na amesikia maombi yetu, afya ya Rais Kikwete inaendelea vyema,” alisema.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: