BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KUNDI LA BOKO HARAM LASABABISHA JESHI LA NIGERIA KUWAHUKUMU WANAJESHI 54 ADHABU YA KIFO.


Wanajeshi 54 wamehukumiwa adhabu ya kifo na mahakama ya Kijeshi nchini Nigeria kwa kukataa kupambana na Wanamgambo wa kiislamu, Boko Haram.

Wanajeshi walikutwa na hatia ya uasi ,kushambulia na uoga.Wanajeshi hao wanashutumiwa kukataa kupigana kurudisha miji mitatu iliyokuwa ikishikiliwa na Boko Haram mwezi Agosti.

Mwanasheria wa Wanajeshi hao amesema wamehukumiwa kifo cha kupigwa risasi na kikosi maalum huku Wanajeshi wengine watano wakiachiliwa.

Vikosi vya kijeshi vya Nigeria vimedai kuzidiwa silaha na Boko Haram, kwa kuwa hawapatiwi silaha za kutosha kupambana na Wanamgambo.

Boko Haram wanapambana kuunda himaya ya kiislamu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.BBC

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: