BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

REAL MADRID MABINGWA WA KOMBE LA DUNIA KWA VILABU 2014, YACHUKUA UBINGWA MIKONONI MWA SAN LARENZO KATIKA ARDHI YA AFRIKA KWA USHINDI WA BAO 2-0..


Mabingwa wa Ulaya Real Madrid wameilaza San Lorenzo ya Argentina katika mchezo wa fainali kwa kuifunga bao 2-0 na kutwaa Kombe la Dunia kwa Klabu
, katika uwanja wa Le Grand Stade de Marrakech nchini Morocco.
Hii ni mara ya kwanza kwa Real kutwaa Kombe hili ambalo ni Mashindano ya FIFA ingawa wameshawahi kutwaa Intercontinental Cup mara 3 ambalo lilikuwa likifanana na hili ingawa hilo lilishindaniwa na Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Mabingwa wa Marekani ya Kusini tu.

Bao za Real hapo Jana zilifungwa na Sergio Ramos na Gareth Bale huku Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, akipata nafasi moja tu ya kufunga ambayo Kipa Torrico aliokoa.


Hivi sasa Real wapo kwenye wimbi la ushindi wa Mechi 22 mfululizo na wanaikimbiza Rekodi ya Dunia ya kushinda Mechi 24 mfululizo inayoshikiliwa na Klabu ya Brazil, Curitiba, waliyoiweka Mwaka 2011.

Real pia wamekamataTaji lao la 4 kwa Mwaka 2014 kitu ambacho walikuwa hawajahi kukifanya baada ya kuwahi kutwaa Mataji Matatu tu ndani ya Mwaka mmoja lakini Mwaka huu 2015 wamefanikiwa kubeba mataji.


Mataji hao ni pamoja na UEFA CHAMPIONZ LIGI, Copa del Rey, UEFA SUPER CUP pamoja na Kombe la FIFA la Klabu Bingwa Duniani. Vile vile wamemaliza Mwaka 2014 kwa kuwa Vinara wa Ligi ya kwao Spain La Liga wakiwa Pointi 1 mbele ya Mahasimu wao FC Barcelona ambao wamecheza Mechi moja zaidi.

Mapema hiyo Jana, kwenye Mechi ya kusaka Mshindi wa 3, Auckland City ya New Zealand iliishinda Cruz Azul kwa Mikwaju ya Penati 4-2 baada ya Sare ya Bao 1-1.


VIKOSI:
REAL MADRID: Iker Casillas, Pepe, Ramos, Marcelo, Carvajal, Kroos, James, Isco, Bale, Ronaldo, Benzema


SAN LORENZO: Torrico, Yepes, Mercier, Buffarini, Kalinski, Cauteruccio, Barrientos, Kannemann, Ortigoza, Mas, Veron

MATOKEO:
Raundi ya Mchujo
10 Desemba - Moghreb TΓ©touan (Morocco) 0 Auckland City (New Zealand) 0[Penati Moghreb 3 Auckland 4]


Robo Fainali
13 Desemba - Entente Setif 0 Auckland City 1
13 Desemba - Cruz Azul (Mexico) 3 Western Sydney Wanderers (Australial) 1


Nusu Fainali
16 Desemba - Real Madrid (Spain) 4 Cruz Azul 0
17 Desemba- San Lorenzo (Argentina) 1 Auckland City 1 [2-1 baada ya Dakika 120]


Mshindi wa 5
17 Desemba – ES Setif 2 Western Sydney Wanderers 2 [Penati 5-4]


Mshindi wa 3
20 Desemba – Cruz Azul 1 Auckland City 1 [Penati 2-4]


FAINALI
20 Desemba - Real Madrid 2 San Lorenzo 0.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: