BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

GARI AINA YA BMW i3 LENYE UWEZO WA KUJIEGESHA KWA KUTUMIA SAA TU TENA BILA DEREVA.

Dereva anaporejea kutoka alikokwenda, analiamrisha gari kutoka sehemu ilikojiegesha na kuja kumchukua dereva.

Hakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako katika jengo la kuegeshea magari lenye gorafa nyingi.


Lakini hivi karibuni hautahihajika kupanda gorofa kutafuta gari lako kwani kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifuaa ambacho kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hiyo kujiegesha yenyewe kwa kubonyeza tu kifaa hicho.


Hata hivyo dereva wa gari hilo atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha.Gari hili linaweza kujiegesha lenyewe kwa kutumia saa ya mkononi ambayo inabonyezwa na dereva.

Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu ya kujiegesha.


Tawi la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua teknolojia hiyo ambayo inawezesha gari kujiegesha lenyewe.


Gari hilo linatumia miale ya Leser iliyo kujitafutia ramani ya jengo ambalo lipo. Dereva anaweza kuliamrisha gari hilo kwenda kujiegesha kwa kutumia Smartphone.

Teknolojia hiyo inajulikana kama ' Remote Valet Parking Assistant,' na inafanyiwa majaribio kwenye gari la BMW i3.


Badala ya kutumia GPS, teknolojia hiyo inatumia miale ya Laser ambayo hutengeza ramani inayolisaidia gari hilo kutafuta sehemu ya kwenda kujiegesha.


Teknolojia hiyo inaiwezesha gari hilo kuona njia na nafasi ya kujiegeshea na pia kuona vizingiti mfano kama magari ambayo hayajaegeshwa vyema.


Kwa mujibu wa waliotengeza gari hilo, linaweza kujitafutia nafasi ya kujiegesha na hata kuweza kutambua sehemu ambako kuna nafasi.

Teknolojia hiyo inatengezwa sambamba na teknolojia nyinginezo zitakazoweza kuzuia gari hilo kugongana na magari mangeine.BBC

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: