Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wakitembea kwenye maji ya mafuriko mtaa wa Madaraka wakati wakitoka eneo moja kwenda lingine desemba 31/ 2014.PICHA/MTANDA BLOG
Ajira ya muda, mwanaume akiwa amemeba mwanamke kwa makubaliano maalum mtaa wa Makongoro. PICHA/MTANDA BLOG
Ajira ya muda, mwanaume akiwa amemeba mwanamke kwa makubaliano maalum baada ya kusindwa kutembea katika maji ya mafuriko katika mtaa wa Makongoro.PICHA/MTANDA BLOG
Mwanaume wa jamii ya kifugaji akiwa na mke wake wakiwa katika makutano ya barabara ya Makongoro na John Mahenge wakivuka maji wakati wakisaka maduka ya kununua bidhaa.
Mkazi wa Manispaa ya Morogoro akitembea kwa tahadhali baada ya mtaa wa Makongoro kuzingirwa na maji ya mafuriko.
Mfanyabiashara wa kuuza ndizi mbivu akiwa ameduwaa baada ya eneo linatumika kuuza aina mbalimbali ya matunda, la kutokea magari soko kuu la mkoa wa Morogoro kujaa maji ya mafuriko.
Ni shida juu ya shida mafuriko yaliyovamia mitaa michache ya Manispaa ya Morogoro Desemba 31/ 2014
Gari likipita mtaa wa John Mahenge kwa kutimua maji ya mafuriko
Mwendesha pikipiki akiwa amekwama na abiria wake mtaa wa Makongoro.
Foleni ya magari jirani na daraja la mto Kikundi barabara ya Korogwe ikiwa imezingirwa na maji ya mafuriko na kusababisha eneo hilo kupitika kwa shida.
Gari la hifadhi ya taifa ya Mikumi Morogoro likiwa limetumbukia katika mtaro mtaa waUhuru.
Mfanyabiashara Chandabay (katikati) akisaidiwa na ndugu zake kuyaondoa maji yaliyoingia dukani kwake mtaa wa Makongoro.
Mwendesha pikipiki akitimua maji na kuzalisha mawimbi wakati akipita mtaa wa Makongoro
Gari ndogo ikipita barabara ya Makongoro Manispaa ya Morogoro.
Soko kuu la mkoa wa Morogoro likiwa limevamiwa na mafuriko desemba 31/ 2014.
Na Habiba Yahya, Morogoro.Mvua
kubwa iliyodumu kwa takribani saa moja na nusu mjini Morogoro jana, imeathiri
miundombinu ya barabara na shughuli mbalimbali zikiwamo huduma za kijamii na
biashara, kusimama.
Mvua hiyo
iliyoanza kunyesha saa 5 asubuhi hadi
saa 6: 30 mchana, ilisababisha barabara za mitaa kadhaa ya katikati ya mji wa
Morogoro kufurika kwa maji.
Hali hiyo
iliathiri usafiri hasa kwa watu wanaotumia pikipiki maarufu kama bodaboda.
Barabara zilizoathirika zaidi ni pamoja na ile
ya Kihonda kwenda katikati ya mjini na Barabara ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine
kwenda Stendi ya Daladala.
Lakini pia
eneo la stendi hiyo pia lilifurika kwa maji ambayo baadaye waliingia ndani ya
magari.
Daladala
zinazotoa huduma kati ya stendi hiyo na maeneo ya Sua, Mazimbu na Kihonda zililazimika kusitisha
shughuli za usafirishaji kwa muda kwa sababu barabara zilikuwa zimekufurika kwa
maji na baadaye foleni kubwa.
Katika eneo
la Kikundi ambako kuna mkondo wa
maji, huduma za usafiri zilisimama baada ya wenye mgari kuhofia magari yao
kusombwa
Mvua pia
imesababisha kuvunjika kwa kuta za daraja lililopo katika Barabara ya Ahmadiya
kuelekea Mtaa wa Ngoto.
.
Pamoja na
mvua hiyo kuathiri shughuli mbalimbali
lakini ilikuwa neema kwa wauza miamvuli ambao walitumia fursa hiyo kufanya
biashara yao mitaani.
Miamvuli
hiyo ilikuzwa inauzwa kwa bei ya juu ikilinganishwa bei ya kawaida katika siku
ambazo hazina mvua.
Mwamvuli
mdogo ulikuwa ukiuzwa kwa bei ya kati ya Sh5,000 na Sh6,000 wakati kwa bei ya
kawaida unauzwa kwa bei ya kati ya Sh2,500 Sh 3,000.
Miamvuli
mikubwa ilikuwa inauzwa kwa bei ya kati ya Sh7, 000 na Sh8000 lakini bei yake
ya kawaida ni kati ya Sh 4,000 na Sh 5,000.
Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
0 comments:
Post a Comment