BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAFUNZI AFUNGWA JELA KWA KUMTUKANA RAIS

Mwanafunzi mmoja nchini Kenya amepewa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kumtukana rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mtandao.

Alan Wadiu Okengo mwenye umri wa miaka 25 pia atalipa faini ya dola 2,200 la sivyo ahudumie kifungo chengine cha mwaka mmoja.

Alikuwa ameshtakiwa kwa kutoa matamshi ya chuki baada ya kusema kuwa watu wa kabila la rais la kikuyu wanafaa kuwekewa mipaka katika maeneo fulani.

Mwanablogu mashuhuri nchini humo pia alishtakiwa baada ya kumwita rais Uhuru Kenyatta 'rais ambaye hajakomaa'.

Kenya ina mitandao mahiri na mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza amesema kuwa kesi hiyo imezua mjadala mkubwa kuhusu kile kilichosahihi katika mitandao.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: