BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIMBA SC KUMBE NI MDEBWEDO KWA MBEYA CITY LIGI KUU TANZANIA BARA, YACHABANGWA BAO 2-0 JIJINI MBEYA.


Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya imeisimamisha Simba SC kwa kuichabanga bao 2-0 katika mchezo mkali wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika jana katika uwanja wa Sokoine jijini humo.





Washambuliaji Paul Nongwa na Peter Malyanzi waliopeleka kilio mwa wekundu wa Msimbazi kwa kupachika mabao katika kipindi cha pili huku wakiweka rehani kuwania nafasi ya pili ya ligi hiyo.

Bingwa mtetezi Azam FC ilifainikiwa kuizima Kagera Sugar kwa kuilaza kwa bao 2-1 kufikisha pointi 42 huku Simba SC ikisaliwa na pointi zake 35.

Katika michezo mingine Polisi Moro SC ilizinduka na kuifumua Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara kwa kuichapa bao 2-0.

Mabao ya Polisi Moro yalipachikwa wavuni na Edward Christopher na Said Bahanuzi dakika ya 60 wakati Christopher akifunga dakika ya 49.

Stend United ilishindwa kutamba mbele ya Ruvu JKT kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: