Abiria 12 wamenusurika kufa baada ya ndege walio kuwa wamepanda kukosea njia na kuingia kwenye nyasi wakati ikitua kwenye uwanja wa karume mjini chake chake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa kusini Pemba kamishina msaidizi Juma Yusufu Ali ametaja ndege ilio kumbwa na tukio hilo kuwa ni AIR SALAMU N0 5H –HAD iliokua ikitokea unguja.
Amesema katika tukio hilo abiria mmoja Mohamed Zahoro Yahaya 21 mkazi wa kichungwani chake chake amepata mshituko na amelazwa katika hospitali ya chake chake.
Dr. wa zamu wa Hospitali ya chake chake Khamisi Masod amesema hali ya abiria huyo wanaendelea na matibabu jamaa wa mjaruhiwa huyo Suleiman Yahaya Suleiman amesema hali ya nduguyake inaendelea vizuri huku akiwa anaendelea na matibabu.
ITV kisiwani Pemba imefika hadi uwanja wa ndege wa karume kisiwani Pemba na kuonana na meneja wa uwanja huo hakuweza kusema chochote na kudai kuwa yeye si msemaji na baadae kupanda ngazi hadi kwa meneja wa mamlaka wa viwanja vya ndege Tanzania TCAA lakini naye akakata kutoa ushirikiano juu ya tukio hilo. ITV
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / Abiria 12 wamenusurika kufa baada ya ndege walio kuwa wamepanda kukosea njia na kuingia kwenye nyasi.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment