BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BREAKING NEWS ! HATARI: A TO Z YA RAIS PIERRE NKURUNZIZA KUPINDULIWA NA JESHI LA NCHI YA BURUNDI LEO PICHA MZIMA NDIYO HII,

18:55 Mwandishi wa BBC aliyeko Dar es Salaam anasema kuwa ndege ya rais Nkurunzinza imepaa ikielekea Bujumbura Rais wa Burundi.

18:53 Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza kufungwa kwa mipaka

18:45 Mwandishi wa BBC huko Bujumbura Kazungu Lozy anasema watu wangali wanasheherekea

18:40 Rais Nkurunzinza ameingia ndani ya gari lake na kuondoka mjini Dar es Salaam akionesha dalili kuwa yuaelekea Burundi Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare

18:37 Kiongozi wa ''Mapinduzi'' kwa upande wake Meja Jenerali Godefroid Niyombare ameamrisha wanajeshi kuzuia rais Nkurunzinza kutua Burundi

18:30 Rais Pierre Nkurunziza anatarajiwa kuhutubia taifa baada ya kurejea kutoka Tanzania amesema msemaji wake Willy Nyamitwe. Wananchi waendelea kusheherekea Bujumbura kufuatia tangazo la ''Mapinduzi''
18:25 Generali Niyombareh ametoa amri kwa majeshi kuungana na kulinda viwanja vya ndege kote nchini humo

18:20 Generali aliyeongoza ''Mapinduzi'' leo asubuhi amewataka maafisa wa jeshi na polisi kufanya kazi kwa pamoja ilikulinda usalama wa nchi hiyo. Rais kikwete alipohutubia waandishi wa habari Dar es Salaam akiandamana na Rais Nkurunzinza

18:15 Viongozi wa kanda ya Afrika wametaka makundi hasimu kutulia na kukubali hali ya kikatiba Kurejea

18:10 Esipisu amesema kuwa rais Uhuru Kenyatta anaunga mkono kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba Maafisa wa jeshi la Burundi wakisheherekea Barabarani Bujumbura

18:07 Msemaji wa rais wa Kenya Manoah Esipisu amesema kuwa viongozi wanataka hali ya kawaida irejee huko Burundi Rais Uhuru Kenyatta akiwa Tanzania
18:06 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi

18:05 Rais amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki

18:01 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''. Raia wakisheherekea ''Mapinduzi''

18:01 Viongozi hao wanakutana dar es salaam kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi

18:01 Rais Jakaya Kikwete amesema hayo katika mkutano wa upatanishi wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki

18:00 Rais wa Tanzania amekashifu ''mapinduzi'' yaliyotoke leo huko Burundi

17:55 Msemaji wa rais Nkurunzinza ameiambia BBC kuwa asilimia 95 ya taifa hilo ingali salama na wala hakuna tashwishi. Manuari za kijeshi zingali barabarani mjini Bujumbura

17:50 Manuari zaidi zaonekana barabarani mjini Bujumbura

17:45 Ujumbe wa mtandao wa facebook wa urais nchini Burundi umekanusha kutokea kwa ''Mapinduzi''.

17:30 Msemaji wa rais Nkurunziza,Willy Nyamitwe ameiambia BBC kuwa rais huyo angali madarakani na kuwa hajaondolewa madarakani Raia wakiwazoma maafisa wapolisi ambao awali walikuwa wakikabiliana nao

17:22 Redio ya taifa ya Burundi inasema kuwa rais Nkurunzinza angali Madarakani na kuwa hakujakuwa na ''mapinduzi'' Raia wakikumbatiana katika bustani la uhuru Bujumbura

17:20 Maafisa wa jeshi wanaolinda kituo cha taifa cha redio wamewaonya watangazaji wasitangaze kuwa kuna ''mapinduzi''

17:05 Mwandishi wa BBC aliyeko huko Ruth Nesoba anasema kuwa waandamanaji wamefululiza hadi kwenye vituo vya polisi na magereza yaliyokuwa na mahabusu waliokamata kwa kuandamana na kuwaachilia huru Wanajeshi ya Burundi wakijaribu kutuliza hali Bujumbura

17:00 Redio ya taifa inasema kuwa bado rais Nkurunzinza angali madarakani.

16:50 Kituo hicho cha redio cha ''African Public Radio'' kinapeperusha tangazo la kupinduliwa kwa serikali ya rais Nkurunzinza Raia wanasherehekea ''kupinduliwa'' kwa Nkurunzinza

16:40 Redio iliyokuwa imefungwa na serikali ya rais Nkurunzinza kwa kupeperusha habari za maandamano imefunguliwa upya.

16:30 Mwandishi wa BBC Cyriac Muhawenay aliyeko Bujumbura anasema raia wanaonekana kuwa na furaha.

16:20 Picha za raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshi Vifaru vya kijeshi katikati ya mji mkuu Bujumbura

16:08 Watu wanaonekana wakininginia kwenye vifaru vya jeshi

16:05 Afisi ya urais nchini Burundi imetangaza kwenye mtandao wake wa twitter kuwa ''hali ni Shwari'' Raia wakishangilia ''mapinduzi''

16:00 Majeshi wameonekana nje ya kambi za kijeshi mjini Bujumbura

15:58 Viongozi wa jeshi wamewaamrisha maafisa wa polisi kuondoka mabarabarani. Raia wakiwa wamekwea vifaru vya kijeshi Bujumbura

15:55 Mwandishi Sonia Rolley, wa Radio France International anasema kuwa halaiki ya raia wamefika nje ya kituo hicho wakishangilia matukio hayo Waandamanaji Bujumbura

15:50 Waandamanaji wanasemekana kuambatana na wanajeshi kuelekea katikati ya mji mkuu wa Bujumbura

15:45 Rais Pierre Nkurunziza ambaye analaumiwa kugombea urais kwa muhula wa tatu, anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, kusikiliza hoja za viongozi wenzake. Waandamanaji Bujumbura

15:40 Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Maud Julien anasema kuwa Miili ya watu watatu imeonekane katika barabara za Bujumbura

15:36 Viongozi wote wa kanda ya Afrika Mashariki na kati wako Dar es Salaam kwa mwaliko wa rais Kikwete. Raia wanashangilia mjini Bujumbura

15:35 Rais Nkurunzinza yuko mjini Dar es Salaam Tanzania kuhudhuria mkutano wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisasa uliokuwa ukiendelea Burundi.

15:30 Maelfu ya raia wa Burundi waandamana a mabarabarani mjini Bujumbura wakishangilia tangazo hilo la ''kutomtambua'' rais Nkurunzinza. Maafisa wa jeshi la Burundi wanaonekana wakiweka usalama

15:20 Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.

15:10 Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza. Maafisa wa polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji wanaopinga hatua ya Rais Nkurunzinza kuwania awamu ya tatu

15:05 Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.

15:00 taarifa zaibuka kutoka Burundi kuwa rais Nkurunzinza ameng'olewa'' madarakani.

Ripoti kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi Polisi wameamrishwa kuondoka mabarabarani

Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.

Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani. Raia wa Bujumbura wakishanilia tangazo la generali Niyombareh

Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.

Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa. Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi

Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.

Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa. Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi

Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.

Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: