BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JOGOO WA SHAMBA AWIKA MJINI KATIKA MASHINDANO YA UMISETA NGAZI YA MKOA MORO 2015.

Winga wa kushoto wa timu ya soka ya halmashauri ya Morogoro Vijijini, Daniel Nobih akiwatoka walinzi wa timu ya Manispaa wakati wa mchezo wa fainali mashindano ya umoja wa michezo kwa shule za sekondari Tanzania (UMISETA) ngazi ya mkoa uwanja wa jamhuri mkoani hapa ambapo katika mchezo huo Manispaa ilifungwa bao 1-0 na Morogoro Vijijini kutawazwa mabingwa Umiseta mkoa wa Morogoro 2015.


Juma Mtanda, Morogoro.
Mashindano ya umoja wa michezo kwa shule za sekondari Tanzania (UMISETA) ngazi ya mkoa yamemalizika kwa wilaya ya halmashauri ya Morogoro Vijijini kuzoa vikombe vingi baada ya kufanikiwa vizuri mkoani hapa.
 
Halmashauri hiyo ilifanikiwa kushinda katika michezo ya soka wavulana na wasichana katika michezo ya fainali huku ikifanya vizuri katika michezo ya basketiboli wavulana na wasichana kwa kutwaa vikombe hivyo.

Wilaya ya Ulanga yenyewe ilibuuka katika ushindi wa jumla katika michezo ya riadha katika mbio fupi na ndefu wakati Manispaa ya Morogoro ilishinda katika mchezo wa mpira wa mikono wavu (Volvo) wavulana na wasichana.

Kwa upande wa wilaya ya Kilombero yenyewe ilitamba katika mchezo wa mpira wa mikono kwa kutwaa vikombe kwa upande wa wavulana na wasichana huku wilaya ya Mvomero ikitwaa kikombe cha nidhamu na mchezo wa netiboli.

Wilaya za Gairo na Kilosa zenye zimeambulia sefuri na kuwa wasindikizaji katika mashindano hayo kwa kushindwa kufanya vizuri na kuondoka bila kikombe chochote.

Baada ya kumalizika kwa michezo hiyo ya Umiseta ngazi ya mkoa wa Morogoro, inatoa nafasi ya kuanza maandalizi ya michezo hiyo ngazi ya kanda ya mashariki ikitarajia kutimua vumbi kati ya Juni 4 hadi Juni 7 mwaka huu katika uwanja wa jamhuri Morogoro.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: