BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KATIBU WA CHAMA CHA MAKOCHA (TAFCA) KUKUMBWA NA ADHABU YA TFF, KISA KUHUSISHA SOKA NA SISA KUPITIA MGONGO WA NKURUNZIZA.

http://oeildafrique.com/wp-content/uploads/2015/05/Pierre-Nkurunziza.jpgShirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limesema taarifa iliyoandikwa na Gazeti moja la tarehe 15, Mei 2015 yenye kichwa cha habari “Nkurunziza ameweka picha mbaya katika soka” haina uhusiano na TFF.

Katika taarifa hiyo katibu wa chama cha makocha nchini (TAFCA), Michael Bundala amenukuliwa akihusisha masuala ya mpira na hali ya kisiasa nchini Burundi.

TFF imesikitishwa na kauli hii na inajitenga nayo. Kwa kua aliyetoa kauli hii ni mwanafamilia ya mpira wa miguu nchini, uongozi wa TFF unafuatilia ili kujua ni hatua gani zichukuliwe.

Jukumu la TFF ni kuendeleza na kusimamia maendeleo ya mpira wa miguu na si vinginevyo.


TFF inawatakia wananchi wa Burundi hususani familia ya mpira, amani, utulivu na baraka katika nchi yao.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: