BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAJESHI WANAOMTII RAIS NKURUNZIZA WAFYATULIANA RISASI NA WALE WA MEJA JENERA NIYOMBORE ENEO LA STATE MEDIA HOUSE BUJUMBURA.


Jeshi limegawanyika, asubuhi hii mapigano makali sana yamezuka mji mkuu wa Burundi kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais na wale watiifu kwa Jenerali aliyepindua.

 
Mapigano hayo yanaripotiwa kuzuka karibu na State media house ambayo toka jana ilikuwa chini ya watiifu wa Rais.

Kumekuwa na mapigano usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi ambako kulikuwa na jaribio la mapinduzi ya kutaka kumng’oa madarakani rais, Pierre Nkurunziza.

Rais huyo ameshindwa kurejea nchini mwake kutoka katika mkutano wa viongozi wa kanda, baada ya ndege yake kugeuza kurejea ilikotokea.


Ingawa askari watiifu kwa rais huyo wamedai kuzima jaribio hilo la mapinduzi yaliyokuwa yakiongozwa na meja jenerali Godefroid Niyombare dhidi ya rais wao na kwamba udhibiti wa nchi uko mikononi mwao na hasa katika maeneo muhimu ya mji mkuu wa nchi hiyo ,Bujumbura.

Makabiliano ya risasi yamesikika karibu na vituo vya redio na runinga. Mwandishi wa BBC aliyeko nchini Burundi amesema kwamba ameshuhudia jeshi likiwa limegawanyika pande mbili na haijulikani nani ameshikilia udhibiti wa nchi kwa sasa.

Rais Nkurunziza amekosolewa kwa haja yake ya kuwania muhula wa tatu wa uongozi nchini Burundi ,maamuzi ambayo yalisababisha wiki kadhaa za maandamano ambapo watu ishirini wameripotiwa kupoteza maisha.
Chanzo: BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: