BRN YAICHONGEA WIZARA YA ELIMU NA KUSABABISHA KAMATI YA BUNGE NA VYAMA VYA UPINZANI KUIFUMUA BAJETI YA WIZARA HIYO BUNGENI DODOMA.
Dodoma. Kambi ya Upinzani Bungeni imeilipua Serikali ikihoji vigezo ilivyotumia kutoa taarifa ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), inayoonyesha kuwa sekta ya elimu imefanikiwa kwa asilimia 81 na kushika nafasi ya kwanza ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mkakati huo.
Imesema wakati takwimu hizo zinatolewa, wanafunzi bado wanakaa chini kwa kukosa madawati, uhaba wa walimu, madarasa na vifaa vya kufundishia, ada juu kwa shule za binafsi, michango lukuki, elimu ya walimu isiyoeleweka, wanafunzi kukosa mikopo, maslahi ya walimu pamoja na kutotekelezeka kwa Sera ya Walimu.
Wakati kambi hiyo ikieleza hayo, Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, imesema hadi kufikia Machi mwaka huu, baadhi ya taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo zilikuwa hazijapata hata senti moja ya fedha ya maendeleo, kikiwemo Chuo Kikuu cha Mzumbe ambacho kilitakiwa kupatiwa Sh850milioni.
Msemaji wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo alihoji; “Ni uwekezaji gani umefanyika hadi tukapata matokeo haya ya BRN? Matatizo yote yanayoikabili sekta ya elimu yameboreshwa vipi? Kuna miujiza gani kama siyo mbinu chafu na ujanja ujanja tu?”
Akifafanua matatizo yanayoikabili sekta ya elimu, Lyimo alisema, “Mwaka 2010 katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM, mliwaahidi Watanzania kuwa kila shule ya msingi itakuwa na darasa la elimu ya awali lenye madawati. Mpaka sasa ahadi hiyo haijatekelezwa hata kwa asilimia 50 tu, watoto bado wanakaa chini na kumeongezeka tatizo la kukosa matundu ya vyoo.”
Alisema mpaka sasa walimu wanaendelea na kilio chao cha malimbikizo ya mishahara na stahili zao nyingine, huku akisisitiza kuwa walimu walioajiriwa Mei Mosi, mwaka huu, mpaka sasa hawajalipwa fedha za kujikimu.
“Tunaitaka Serikali kuonyesha fedha zilizotengwa kwa ajili ya nyongeza ya mishahara ya walimu katika bajeti ya 2015/16. Tunataka kujua walimu zaidi ya 37,000 waliopandishwa madaraja lakini hawajarekebishiwa mishahara yao watalipwa lini?” alisema Lyimo.
Aliiponda sera mpya ya elimu iliyozinduliwa na Serikali hivi karibuni kuwa haiwezi kufanikiwa, alisema kuna mambo matatu yanayoweza kuifan
Kuhusu upanuzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, alisema makandarasi wametishia kukipeleka mahakamani kutokana na kushindwa kuwalipa Sh1.2 bilioni za ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ambao ulikamilika toka 2009.
Kamati hiyo pia iliishauri Serikali kuhakikisha inawaandaa wataalamu kwa ajili ya kutoa elimu bora kwa wanafunzi, kuboresha mazingira ya walimu na kuondoa kero za utolewaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, waziri wake Dk Shukuru Kawambwa aliomba kuidhinishiwa Sh989.5 bilioni kwa mwaka 2015/16.
Wabunge
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Diana Chilolo alichafua hali ya hewa baada ya kuwapiga vijembe Chadema kuwa ni afadhali nyumba yake kuliko jengo la makao makuu ya chama chao.
Chilolo aliwapiga vijembe hivyo wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo ya elimu.
“Mmeshindwa hata kujenga barabara ya kwenda ofisini kwenu kwa kiwango cha lami yaani mita 100 tu zinawashinda,” alisema na kuamsha hasira za wabunge wa Chadema waliosimama wakitaka Mwenyekiti wa Bunge, Lediana Mngo’ngo awape nafasi wampe taarifa.
Hali hiyo iliwafanya Halima Mdee (Kawe-Chadema) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini-Chadema) kusimama lakini hawakupewa nafasi.
Hata hivyo, alipopewa nafasi Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo alimtaka mbunge huyo kutosema jambo bila ya kuwa na uhakika.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Felister Bura alisema ni muhimu kwa Serikali kuhakikisha kuwa walimu wanalipwa madai mbalimbali wanayoyadai.
Felister alisema walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu, wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la kipekee. Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Rachel Mashishanga alisema kuna tatizo katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Alisema baadhi ya wanafunzi hususan wasio na uwezo, hukosa mikopo huku wale wenye uwezo wakipata.
ya ifanikiwe ambayo ni kuwa na walimu bora, zana bora za kufundishia na walimu wenye motisha, huku akiitaka Serikali kueleza imetenga fedha kiasi gani ili kufanikisha mambo hayo matatu.
“Tunataka kujua ni lini elimu ya msingi katika mfumo wa umma itatolewa bure kama inavyoeleza sera ya elimu,” alisema.
Katika hotuba hiyo, kambi ya upinzani ilihoji baadhi ya vyuo kuanza kujitengenezea mitalaa yake kwa lengo la kuwavutia wanafunzi, jambo linalosababisha kukosekana kwa ubora linganifu wa elimu ya juu katika ngazi mbalimbali.
Akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii, Mwenyekiti wake Margaret Sitta alieleza changamoto lukuki zinazoikabili Wizara ya Elimu.Mbunge wa Kuteuliwa (NCCR-Mageuzi), James Mbatia alisema zinahitajika juhudi za makusudi katika kuhakikisha kuwa elimu inapewa kipaumbele. Alisema elimu nchini bado iko chini kunahitajika juhudi za kutosha kuiokoa.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment