MAAFISA WA JESHI LA POLISI WASHAMBULIWA NA 11 KUJERUHIWA.
Kumekuwa na msururu wa mashambulizi ya maguruneti kuwalenga maafisa wa polisi katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura.
Maafisa wa usalama wanasema kuwa takriban polisi 11 walijeruhiwa usiku kucha.
Maguruneti hayo yalirushwa katika maeneo ambayo yaliathiriwa na maandamano ya ghasia kufuatia hatua ya rais Pierre Nkurunziza kutaka kuwania muhula wa tatu.
Maafisa wa polisi wamewalaumu wanaharakati wa upinzani.
Makundi ya haki za kibinaadamu yanasema takriban watu sabini wameuawa na wengine 500 kujeruhiwa tangu maandamano hayo yaanze mnamo mwezi Aprili.
0 comments:
Post a Comment