BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKAPA AANGUSHWA NA WILLIUM MKOANI MTWARA.

Matokeo ya kura za maoni kugombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) yameendelea kutangazwa na kuwatupa nje baaadhi ya viggo na sura mpya kuibuka.

Katika Jimbo la Nanyumbu, mkoani Mtwara, Willium Dua alitangazwa mshindi kwa kupata kura 6,165 huku mpinzani wake wa karibu Yahya, Mhata akipata kura 6,157.


Mbunge anayemaliza muda wake, Dastan Mkapa, alishika nafasi ya tatu 9,3945. Wengine ni Endrick Napacho kura 2,096, Majaribu Lupeto kura 931, Uledi Mwanache 497 na Hassan Wema kura 296.


JIMBO LA KIBAMBA

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mkangara, ameibuka kidedea baada ya kupata kura 5,576 akifuatiwa na Issa Mtevu kura 3,296.

Nafasi ya tatu ni John Hugo aliyepata kura 319 na Pendo Kujerwa alipata kura 309.


JIMBO LA KAWE

Kippi Warioba ameibuka mshindi baada ya kupata kura 5,212 akifuatiwa na Coleman Massawe kura 4,280, Juma Pijei 2,497 na John Cornel kura 584.

Katika jimbo hilo, wanahabari Abdallah Majura na Jerry Muro wameangushwa.


JIMBO LA UBUNGO

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi, amepata aliongoza kwa kura 6,068, Kalist Lyimo 2,808, Hawa Ng’humbi 1,772 na Jordan Balindo kura 212.

JIMBO LA KINONDONI

Idd Azan amefanikiwa kutetea nafasi yake baada kupata kura 6,479, Michael Wambura 1,212, Wangota Salum 1,149 na Joseph Mhonda kura 751.

JIMBO LA ILALA

Mbunge anayemaliza muda wake Mussa Zungu ametetea nafasi yake kwa kupata kura 10,457 akifuatiwa na Mkuu wa zamani wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo kura 2,038 na Waziri Kindamba kura 575.

JIMBO LA UKONGA

Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa amepata ushindi wa kura 10,000 dhidi ya Raesh Patel kura 7,356 na Rober Masegesi kura 548.

JIMBO LA SEGEREA

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk.Milton Mahanga ameangushwa na Bonna Kaluwa kura 6965.
Dk. Mahanga alipata kura 2,381 na Scolastica Kevila kura 6,155.

SONGEA MJINI

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, ameibuka kidedea katika jimbo la Songea Mjini kwa kupata kura 6,287 na kumshindwa mpinzani wake wa karibu Waziri Nchi wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huviza, kura 5,600.

Mussa Gama alishika nafasi ya tatu baada ya kupata kura 1,278a akifuatiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Namtumbo, Azizi Fakiri kura 1,101.


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST), Erick Mapunda alipata kura 908, Meneja Masoko wa Clouds FM Radio, Raymond Mhenga 576, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Francis Miti kura 475 na Wakili wa Kujitegemea Manispaa ya Songea, Sebastian Waliyuba kura 265.


JIMBO LA MAKETE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Binillith Mahenge, ametetea nafasi yake katika jimbo la Makete baada ya kuibuka mshindi mwembamba.

Dk. Mahenge alipata kura 8,534 dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk. Norman Sigala alipata kura 8,211, Bonic Muhami kura 500, Fabianus Mkingwa, 466 na Lufunyo Rafael aliyepata 226.


JIMBO LA MUFINDI KUSINI

Katika jimbo la Mufindi Kusini lililokuwa na wagomba 14, Mendra Kigola aliibuka kidedea baada ya kupata kura 7,511 akifuatiwa na na Dickson Lutevele kura 3,210, Albert Chalamila kura 1,898, Marcelina Mkini 1,684, Mary Miho 413, Antony Mpiluka 331 na Wendei Ng’ahali kura 298.

JIMBOLA MUFINDI MJINI

Cosato Chumi alipata ushindi kwa kupata kura 3,686, Zuberi Ngullo kura 700, James Mgimwa kura 408 na Benjamini Billali kura 312.

JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI

Jimbo la Mufindi Kaskazini,Mahmoud Mgimwa alipata ushindi wa kura 12,235, nafasi ya pili ikishikiliwa na Exaud Kighahe kura 2,343, Raphael Kalinga kura 1520 na Godfrey Ngupula kura 980.


JIMBO LA ARUSHA MJINI

Mshindi ni Philemon Monaban (5,320) akifuatiwa na Justin Nyari (1894), Moses Mwizarubi (1005), Reuben
Mwiteni (171), Thomas Munisi (832),Victor Njau (752), Emmanuel Ole Njoro (90),Mohammed Omary (171), Swalehe Kiluvia (446), Hamisi Migire (305), Weraufoo Munisi (832) na Mustafa Panju (498).

JIMBO LA NGORONGORO

Mshindi ni William Ole Nasha (30,389), Elias Ngorisa (15,599), Dk. Eliamini Taika (10,588), Saning’o Ole Telele (6,432), Patrick Kasango (3,222) naJoseph Saitoti (2,384)

ARUMERU MANGHARIBI


Mshindi ni ni Loi Sabaya (10,321), , Furaha Lekoko ,

8,450), Elisa Mollel
(3,253), Daud Molle (2,183), na Henry Mejooli (2,025) na 0 Osiligi Losai (1,206).

LONGIDO

Mshindi ni Joseph Kuruju (5,452), Lomayani Kodie (4,579) na Philip Kitaso (4,096).

Imeandikwa na Hussein Ndubikile; Juma Mohamed, Gideon Mwakanosya, Furaha Eliabu, George Tarimo na Cyanthia Mwilolezi.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: