BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAZIRI WA MIFUGO NA MAENDELEO YA UVUVI AMTWANGA MAKONDE MSIMAMIZI WA UCHAGUZI KATIKA KURA ZA MAONI BAADA YA KUSHINDWA MJI MDOGO WA BUSEGA.

 
Hali ya mtafaruku iliibuka jana wakati aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani, alipogeuka bondia kwa kumpiga makonde msimamizi wa uchaguzi , Jonathan Mabihya.
Baada ya kutangazwa kushindwa kwa uchaguzi wa marudia wa kura za maoni.

Dk. Kamani amebwagwa na Raphael Chegeni ambaye alikuwa mpinzani wake mkubwa katika uchaguzi huo.
Hata hivyo, Dk. Kamani alipotakiwa kueleza sababu ya shambulio hilo, hakutaka kueleza na badala yake alisema hakutendewa haki.

Katika valangati hilo, Dk. Kamani alipata hasara baada ya kuvunja miwani yake kutokana na ngumi yake ya mkono wa kulia kumkosakosa msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa CCM wilaya ya Meatu. 


Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani.
Wakati Mabihya akitaja jina la Dk. Chegeni kama mshindi, miwani ya Dk. Kamani ilidondoka wakati akimsindikiza kwa konde la mkono wa kulia katibu huyo.

Hali hiyo ilisababisha polisi kuingilia kati ili kuokoa purukushani hiyo na kurudisha hali ya amani.

Vurugu hizo zilizodaiwa kuanzishwa na Dk. Kamani na wafuasi wake, zilisababisha viongozi wa CCM waliokuwa wakisimamia uchaguzi huo kabla ya matokeo kutangaziwa kuondoka ofisi za chama hicho wilaya ya Busega wakisindikizwa na polisi.

Mawaziri ambapo mpaka sasa wamebwagwa katika uchaguzi huo ni pamoja na Mathias Chikawe, (Mambo ya Ndani), Gaudentia Kabaka (Kazi na Ajira) na Dk Seif Rashid (Waziri wa Afya) wakati Manaibu ni wa Fedha Adam Malima, Maji, Amos Makala, na Makongoro Mahanga wa Kazi na Ajira.

JIMBONI UKONGA
Meya wa Ilala Jerry Slaa, amemshinda mpinzani wake Rashed Patel kwa kura 10,965 dhidi ya 6,960 alizopata .

Uchaguzi wa jimbo hilo ulirudiwa baada ya matokeo ya awali kulalamikiwa. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: