BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHADEMA YAPATA HASARA KWA KUKIMBIWA NA WAENEZI WAO NA KUTIMUKIA CCM KATIKA MIKOA YA DODOMA NA MTWARA.

Mweyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Picha ya Maktaba.

Ndugu Peter Chiuyo Mkurugenzi wa habari na uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Dodoma ahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuona ubabaishaji mwingi ndani ya Chama hicho.

Mwenezi huyo wa Mkoa wa Dodoma amejiunga rasmi na CCM alasir ya leo tarehe 2/9/2015 katika viwanja vya Chang'ombe, Dodoma mjini na kupokelewa na mgombea mwenza wa CCM, Mhe Samia Suluhu ambae ameendelea na Kampeni katika Mkoa wa Dodoma.

Wakati huo huo, Mwenezi wa CHADEMA Mkoa wa Mtwara akiongozana na wanachama 50 wa chama hicho wajiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa hadhara wa Mgombea Urais wa CCM ndugu John Pombe Magufuli uliofanyika katika uwanja wa mashujaa, Mtwara mjini na kurushwa (live) na vituo vya televisheni kikiwemo Star TV.

Yawezekana SLAA alikuwa ni ASSET ndani ya CHADEMA...tusubiri kusikia zaidi.CHANZO:http://www.jamiiforums.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: