BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JANUARY MAKAMBA, DEO FILIKUNJOMBE WAKUWAA KISIKI MBELE YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC).


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imepitisha rufaa 13 zilizokuwa zimewekewa pingamizi za kugombea ubunge katika baadhi ya majimbo nchini yakiwamo ya Ludewa la Deo Filikunjombe (pichani kushoto), mkoani Njombe na Bumbuli mkoani Tanga linalotetewa na Januari Makamba.

Akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam Ofisa wa Tume, Athumani Masesa, alisema uamuzi huo umetolewa baada ya kusikiliza rufaa 40 kati ya 56 zilizowekewa pingamizi. Makamba na Filikunjombe ni miongoni mwa wagombea waliotarajiwa kupita bila kupingwa baada ya kuwawekea pingamizi wapinzani wao, hasa kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Alisema tume hiyo ilitulipia mbali pingamizi nyingine 27 baada ya kupitia maelezo na kubaini kuwa hazikuwa na hoja za msingi za kuishawishi .

Aliyataja majimbo mengine kuwa ni Bumbuli ambalo mgombea wake wa CCM, January Makamba, Peramiho la mgombea wa chama hicho, Jenister Mhagama na Ludewa la Deo Filikunjombe.

Alisema Nec leo inatarajia kuendelea kupitia rufaa nyingine zilizobakia na baada ya kukamilisha kazi hiyo, wataanza kupitia 196 za madiwani kwa ajili ya maamuzi.

Awali waliotangazwa kupita bila kupingwa ni Makamba, Rashid Shangazi, Abdallah Chikota(Nanyamba) na Filikunjombe. SOURCE: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: