BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTU MOJA AFARIKI DUNIA KATIKA MKUTANO WA KAMPENI, JK AMNADI MGOMBEA URAIS WA CCM DK MAGUFULI KATIKA UMATI WA WANANCHI UWANJA WA JAMHURI MORO.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dr. Jakaya Kikwete akizungumza katika mkutano wa kumnadi mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri katika Manispaa ya Morogoro mkoani humo ambapo maelfu ya wananchi mjini Morogoro wamehudhuria katika mkutano huo.

Dr. John Pombe Magufuli amewaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu na kumchagua ili aweze kuwatumikia watanzania kwa ujumla wake na kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo ya watanzania ili kuipaisha Tanzania katika maendeleo.

Ameongeza kwamba yeye atakuwa rais wa watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama, Makabila, Dini wala Ukanda kwani maendeleo hayana vyama, Kabila, Dini wala Ukanda ila ni kwa watanzania wote.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MOROGORO)

Katika tukio la kusikitisha baada ya kumalizika salama mkutano huo wa kampeni, mtu mmoja amefariki dunia na wengine zaidi 10 kujeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro baada ya kutokea vurugu huku baadhi ya watu wakianguka chini katika langu kuu la uwanuja wa jamhuri wakati wakitoka nje.

Tukio hilo lilitokea baada ya msafara wa Dk Magufuli kutoka na watu kurundikana mlango hali iliyotoa nafasi ya watu kusukumana hovyo na kupelekea baadhi yao kuanguka chini na kukanyagwa.

Habari zaidi la tukio hilo litalipotiwa zaidi na MTANDA BLOG.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wakati alipowasili kwenye uwanja wa jamhuri kwa ajili ya mkutano wa kampeni.



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dr. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wakiwapungia mikono wananchi huku wakiwa wameshika kofia zao.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dr. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wakifuatilia jambo huku wakiwa na sura za tabasam wakati Mzee Yusuf Makamba akihutubia wananchi mkoani Morogoro kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Bw. Innocent Kalogeres.




Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mkoani Morogoro na kuomba kura kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani humo.



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akisistiza jambo katika mkutano huo.



Maelfu ya wananchi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.





Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro mjini Mh. Mohamed Abood.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimkabidhi ilani ya Uchaguzi mgombea ubunge wa jimbo la Morogoro mjini Mh. Abdullaziz Mohamed Abood.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa CCM Ndugu Abdallah Bulembo akiwahutubia wananchi wa Morogoro katika mkutano huo.



Mwenyekiti wa CCM Mh. Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mzee Yusuf Makamba.



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dr. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wakiimba wimbo katika mkutano huo kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Bw. Innocent Kalogeres.



Mzee Yusuf Makamba akiwahutubia wananchi wa Morogoro katika mkutano huo.



Msanii Ali Kiba akifanya vitu vyake jukwaani katika mkutano huo.







Kundi la Wasanii wa Filamu nchini la Mama Ongea na Mwanao likitumbuiza katika mkutano huo.





Kundi la muziki la TOT likitumbuiza katika mkutano huo.



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akipunga mikono kwa wananchi waliofurika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati akiwasili uwanjani hapo.



Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wakimpokea Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wakati akielekea mjini Morogoro.



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi akiwa njiani kutoka Ifakara kwenda Kilosa mkoani humo.



Baadhi ya watoto wakiwa wameshikilia picha ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni mjini Kilosa.



Baadhi ya Watawa wakifurahia jambo wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akizungumza mjini Mikumi.



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mlimba Bw.Godwin Emmanuel Kunambi.



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombeaJonas Estomih Nkya.



Mmoja wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo akifurahia jambo.



Wananchi wa Kilombera wakinyanyua mabango yao juu juu wakati wa mkutano huo.



“Hapa ni Kazi tu”



Steven Nyerere anakamua tu hapo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: