Wakazi
wawili wa jijini Dar es Salam, wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka kumi yakiwamo ya kughushi na
kutengeneza tovuti bandia zenye majina ya viongozi mbalimbali akiwemo
Rais Jakaya Kikwete.
Washtakiwa hao ambao ni Maxmillian Msacky na Patrick Natala
wanadaiwa kutengeneza tovuti bandia kwa kudai zinamilikiwa na viongozi
Jakaya Kikwete Foundation (Ikulu), Taasisi ya Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA Foundation) na kampuni ya Jamii ya Kuweka na Kukopa ya
Akiba (Akiba Saccos Social Company).
Nyingine ni kampuni ya Jamii ya Ridhiwani (Ridhiwani Social
Company), Hisa Tanzania, Taasisi ya Zitto Kabwe (Zitto Kabwe
Foundation), Vicoba Tanzania na Mfuko wa Wekeza (Wekeza Fund).
Mwendesha mashtaka wakili wa serikali mkuu, Theophil Mutakwawa,
akisaidiana na Shadrack Kimaro na Jackline Nyatori, walidai katika mahakama hiyo kuwa tarehe tofauti ya mwezi Januari na Aprili, 2014, jijini
Dar es Salaam, walitengeneza mfumo wa mtandao uitwao Hisa Tanzania,
mahususi kwa ajili ya kulaghai.
Katika shtaka la pili washtakiwa wote kwa kutumia miundombinu ya
mtandao huo, walitengeneza tovuti ijulikanayo kama Jakaya Foundation,
yenye lengo la matumizi ya kulaghai.
Aidha, walitengeneza mfumo wa mtandao uitwao Ridhiwan Social
Company, washtakiwa hao pia walitengeneza mfumo wa mtandao uitwao TCRA
Foundation.
Katika shtaka la tano, tarehe isiyojulikana kati ya mwaka 2001 na
2014 mshtakiwa Msacky akiwa na nia ya kulaghai au kudanyanya, alighushi
cheti cha elimu ya Sekondari namba 0421130 chenye index namba
S02360-0010 akiwa na lengo la kuonyesha cheti hicho kilikuwa halali na
kimetolewana Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), huku akijua kuwa si
kweli.
Ilidaiwa katika shtaka la sita, tarehe isiyojulikana kati ya mwaka
2005 na 2014, mshtakiwa Msacky, alighushi alighushi cheti cha kidato cha
sita namba 0217951 chenye index namba S0310-0532, akiwa na lengo la
kuonyesha cheti hicho kilikuwa halali na kimetolewa NECTA huku akijua
kuwa siyo kweli.
Katika shtaka la saba, tarehe isiyojulikana, kati ya mwaka 2006 na
2014, mstakiwa huyo alighushi cheti chenye namba 2004-120202, kwa lengo
la kuonyesha cheti hicho kilikuwa halali na kimetolewa na Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, kitengo cha kompyuta.
Katika shtaka la nane, tarehe isiyojulikana, kati ya mwaka 2010 na
2014, mshtakiwa huyo akiwa na nia ya kulaghai au kudanganya, alighushi
Nakala ya Kitaaluma ikiwa na usajili namba 7703/T.07, kwa lengo la
kuonyesha nakala hiyo ilikuwa ni halali na imetolewa na Chuo cha Mzumbe,
huku akijua nim uongo
Mahakama hiyo ilielezwa kuwa, katika shtaka la tisa, tarehe
isiyojulikana, kati ya mwaka 2010 na 2014, mshtakiwa huyo, alighushi
Cheti cha Chuo chenye namba za usajili 6109 kwa lengo la kuonyesha,
cheti hicho ni halali na kilitolewa na chuo cha Mzumbe, wakati
akitunukiwa Shahada ya kwanza ya Sayansi katika Menegimenti ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, huku akijua kuwa si kweli.
Katika shtaka la kumi, ilidaiwa kuwa mwezi Julai, 2014 katika ofisi
ya SB Enterprises , zilizopo barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam,
mshtakiwa Msacky, kwa nia ya kudanganya, ili kulinda ajira alitoa
nyaraka mbali mbali za uongo za vyeti hivyo, kwenye kampuni hiyo,
kuonyesha kuwa ni za halali na zimetolewa na mamlaka husika, huku
akijua kuwa taarifa hizo siyo za kweli.
SOURCE:
NIPASHE

0 comments:
Post a Comment