BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SIASA ZA UCHAGUZI MKUU 2015: MGOMBEA URAIS UKAWA, EDWARD LOWASSA NA MHE FREDERICK SUMAYE NI VIONGOZI MIZIGO ISIYOBEBEKA KAMA LUMBESA.


‘Losassa, Sumaye ni mizigo mizito’
 


JUMUIYA ya Umoja wa Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) imesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) muda mfupi ujao kitajutia uamuzi wa kumkaribisha Waziri Mkuu aliyejiuzu, Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye kwa sababu viongozi hao ni mizigo isiyobebeka kama lumbesa.

Matamshi hayo yalitolewa juzi na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Isimani, William Lukuvi, uliofanyika kwenye viwanja Kata ya Kihorogota mkoani hapa.

Shaka alisema uamuzi wa chama hicho kuwachukua viongozi hao haukufanyiwa upembuzi makini na yakinifu na kwamba uamuzi aidha ya Chadema na Ukawa ikiwa wanafikiri wamepata mtaji wajijue wamepatikana.

Alisema viongozi hao wamepoteza haiba na mvuto wa kuwa viongozi wenye heshima, amana na uadilifu mbele ya jamii iliozoea kuongozwa kwa uzingatiaji wa misingi ya adabu, utii na uaminifu.

"Nawapa pole sana viongozi wa Chadema na Ukawa kwa kukukubali kupokea viongozi mizigo mizito kuliko lumbesa, hawabebeki na wamepoteza haiba ya heshima mbele Watanzania," alisema Shaka.

Shaka alisema uongozi wa nchi unahitaji mgombea na kiongozi mwaminifu, mtiifu na mzalendo ambaye hana shutuma wala tuhuma za ufisadi au ubadhirifu wa mali za umma.

Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema CCM inashukuru sana viongozi hao kuhama kwa sababu walikuwa wakikitia madoa na ingekuwa kazi kufanya kampeni za kuomba kura kama Lowassa na Sumaye wangebaki CCM.

Aidha, Shaka aliwataka wananchi wa Isimani kutopoteza muda wao wa kukishabikia chama cha siasa kama Chadema ambacho hakina sera, malengo, dira wala mipango na mikakati ya kushika hatamu za utawala wa dola na kusimamia maslahi ya umma.

Shaka pia aliponda sera ya majimbo ya Chadema na kuiita ‘sera hatari’ kwa mustakabali wa amani ya nchi na umoja wa kitaifa, utulivu yenye nia ya kuibua ubaguzi na ukabila.

“Ikataeni Chadema kwa sababu ina sera ya majimbo inayoweza kuligawa taifa na kulijengea matabaka ya ukabila, ukanda na kuvuruga misingi; isiyoheshimu usawa na haki," alisema Shaka.

Aliwahimiza wananchi wa Isimani kumuunga mkono na kumchagua mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, akimtaja kama kiongozi anayekubalika, kuheshimika na kuaminika katika utendaji na usimamiaji wa majukumu yake katika wizara alizokabidhiwa na serikali.

Shaka aliwataka wanancni wa Jimbo la Isimani kuendelea kumchagua Lukuvi ambaye ni kiongozi hodari, mchapakazi, jasiri anayependa kuwajali watu, kuwathamini na kuwatumikia.CHANZO:www.raiatanzania.co.tz
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: