TIMU YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 15 ILIVYOJIKUA KATIKA VISIKI VYA MORO KIDS NA MORO KOMBAINE UWANJA WA JAMHURI MOROGORO.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15, Mohamed Ally Makamba kulia akiwania mpira na mlinzi wa timu ya vijana wenye umri huo ya Moro Kombaine Athman Isihaka wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa jamhuri Morogoro, Timu hizo zilitoka suluhu.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa 15 imekuwaa kisiki katika kichezo yake ya kujipima nguvu dhidi ya Moro Kids na Moro Kombaine katika michezo yake ya kujima nguvu iliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Katika michezo hiyo, timu ya taifa vijana iliweza kuambulia sare ya bao 1-1 mbele ya Moro Kids huku katika mchezo mwingine ikilazimishwa suluhu.
Mshambuliaji wa Moro Kids, Boniface Joseph aliokoa jahazi la timu yake isilale mbele ya wenzao kwa kupachika bao la kusawazisha dakika ya 37 kufuatia mpira wa kona uliochongwa na Frank George huku bao la mapema lililopachikwa na Alex John dakika ya 27 liliwapa matumaini ya ushindi.
Bao hilo lilipatikana baada ya kumiminwa vyema kona iliyochongwa na Mohamed Ally na kumkuta mfungaji aliyenga bao hilo na kufanya mchezo huo umalizike kwa sare ya bao 1-1.
Timu hiyo ya vijana inayonolewa na Kocha Mkuu Bakari Shime ilijitopa tena uwanjani leo (jana) kucheza na Moro Kombaine lakini mchezo huo ulimalizika kwa sululu.
Baada ya kumalizika kwa michezo hiyo miwili katika mkoa wa Morogoro wachezaji wa timu ya taifa watarejea Dar es Salaam ambapo kambi itavunjwa ili wachezaji hao kuendelea na masomo.
Timu hiyo inaandaliwa kwa ajili kucheza mechi za kufuzu Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2017 na kila wiki ya mwisho wa mwezi wamekuwa wakikutana kwa mazoezi na michezo ya kujipima nguvu.
Katika michezo miwili iliyofanyika katika mkoa wa Morogoro, timu hiyo ya vijana imejikuta ikikuwaa kisiki kwa mara ya kwanza kumaliza dakika 90 bila ushindi tangu waanze programu hiyo Juni mwaka huu, wakishinda mechi zote zao Mbeya na Julai Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment