MKE NI SAWA NA TV NA MCHEPUKO NI SAWA NA SIMU !!.
KUTOKA KWA Juma Michael Mwanaharakati.
MKE ni sawa na TV na mchepuko ni sawa na SIMU....nyumbani unaangalia TV lakini ukitoka unatoka na SIMU. Mara chache unafurahia TV lakini Muda mrefu unacheza na SIMU yako.
TV ni bure kwa maisha yako yote, lakini SIMU kama hujalipia hupati huduma. Gharama za huduma za TV ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za SIMU ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.
TV ina remote lakini SIMU haina.
Kitu muhimu zaidi, SIMU ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini TV unalazimika kusikiliza tu na kuona hata kama hutaki au unataka. Unaweza kununua TV mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini SIMU mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.
Ya mwisho na ya kuzingatia zaidi katika maisha TV haina virusi lakini simu ina virusi.
0 comments:
Post a Comment