BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SOKWE AZALISHWA MTOTO KWA NJIA YA UPASUAJI NA PROPESA AMBAYE AMEWAZALISHA WANAWAKE.

 

Mwana wa Sokwe anaendelea vyema baada ya kuzaliwa kupitia upasuaji katika hali isiyo ya kawaida.

Sokwe huyo anayetoka upande wa magharibi alizaliwa kupitia upasuaji usio wa kawaida baada ya mamaake kuonyesha ishara za ugonjwa hatari wa shinikizo la damu.

Alihitaji msaada wa kupumua, lakini sasa madaktari wanasema hali ya mama na mtoto iko shwari.

Madaktari wakimzalisha sokwe kwa njia ya upasuaji  

Kumekuwa na sokwe wachache waliofanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua duniani, kisa cha hivi majuzi kikiwa kile cha San Diego Safari Park mwaka 2014.

Sokwe huyo aliye na siku 11 alizalishwa na Professa David Cahill ambaye amewazalisha wanawake wengi kupitia upasuaji ,lakini ilikuwa mara yake ya kwanza kumzalisha sokwe.
''Mbali na kuwa na watoto wangu,huu ni ufanisi mkubwa kwangu,kitu ambacho sitoweza kusahau tena,''alisema.

Aliulizwa maoni yake baada ya mamaake sokwe huyo kwa jina Kera kuugua ugonjwa wakati ambapo alikuwa karibu kujifungua.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: