BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAFANYABIASHARA WA SIMU WAOMBA SERIKALI KUONGEZA MUDA WA KUZIMA SIMU FEKI.

Wakati tarehe kumi na saba juni mwaka huu simu zote feki zikitarajiwa kuzimwa baadhi ya wafanyabiashara za simu za mikononi katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam walalamikia kukosa kabisa wateja na kupata hasara kubwa kutokana na kuwa na simu nyingi ambazo ni feki.

Wakati wafanyabiashara wakilalamika kupata hasara, upande wa watuamiaji nao wamelalamika kuwa watakosa mawasiliano kutokana na simu origino kuwa ghali. 

Siku chache baada ya mamalaka ya mawasiliano nchini TCRA kuonesha msimamo wake wa kuzifungia simu hizo baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam wameelezea kuwa katika wakati mgumu kutokana na kukosa wateja na hivyo kusababisha hata simu ambazo sio feki kukosa wateja.


Wafanyabiashara wabaini kupata hasara kubwa kutokana na azimio hilo ambapo wameziomba mamlaka husika kuongeza muda ili kuwapa nafasi ya kujipanga ili kutafuta mtaji wa kuingiza simu zinazotakiwa.

Baadhi ya watumiaji waliozungumza na ITV nao wameitupia lawama serikali kwa kutoa agizo la kuzimwa kwa simu feki huku ikiruhusu simu hizo kuingia nchini na kuzitaka mamlaka husika kulitizama upya swala hilo ama kuweka bei elekezi kwa simu halisi ili iwe rahisi kwa wananchi wa kipato cha chini kuzinunua.

Wapo baadhi ya wauzaji wa simu pia walioipongeza serikali kwa hatua iliyochukuwa ya kuzima simu feki na walikuwa na haya ya kusema.

Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA tayri imeonesha msimamo na kutangaza kuwa tarehe kumi na saba juni mwaka huu simu zote feki zitazimwa ikumbukwe kuwa zoezi la kufungiwa kwa simu feki sio geni kwa nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya ambao tayari wameshazifungia kabisa simu feki.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: