BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAFANYAKAZI WATATU NGAZI YA JUU WA MAMLAKA YA MAWASILIANO WANG'OLEWA KAZINI.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewasimamisha kazi na kuwastaafisha maofisa watatu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa tuhuma za kuhujumu mtambo wa mawasiliano na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni nne.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu, Profesa Mbarawa aliwataja maofisa hao kuwa ni Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Elizabeth Nzagi, Mwanasheria Modester Ndunguru na aliyekuwa msimamizi wa mtambo huo, Mhandisi Richard Sunday.

Alisema kuna kifaa cha kubaini gharama za mawasiliano ya kila simu nchini ili kujua kampuni zinapata kiasi gani kilipaswa kufungwa kwa muda mrefu, lakini hakikufugwa kwa sababu zisizojulikana.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
“Mkataba ulisema kifugwe ili tujue gharama za mawasiliano lakini hakikufugwa na badala yake kujua gharama imetegemea kampuni za simu pekee, huku simu za nje serikali ikijua gharama husika,” alisema.

Alisema maofisa hao watakuwa nje ya vituo vyao vya kazi wakati uchunguzi ukiendelea kwa hatua zaidi. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: