HABARI MPYA ! MHARIRI MTENDAJI WA MAGAZETI YA SERIKALI ATENGULIWA CHEO CHAKE NA RAIS MAGUFULI.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli ametengua uteuzi wa Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Gabriel Nderumaki pichani.
Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 14 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, taarifa hiyo kutoka Ikulu imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Machi, 2016.
Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Tuma Abdallah kukaimu nafasi hiyo.
Tuma Abdallah ni Mhariri Mtendaji Msaidizi wa Magazeti ya Serikali (TSN)
0 comments:
Post a Comment