Mwanamuziki Papa Wemba, chini ni video aliyoanguka na kupoteza fahamu kisha kufariki duniani akiwa jukwaani
Dar es Salaam. Mwanamuziki nguli wa Bolingo kutoka Demokrasia ya Congo, Jules Shughu Wembadio Pene Kikumba maarufu kwa jina la Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast akiwa jukwaani.
Taarifa za awali kutoka kituo cha Utangazaji cha France 24 zinasema kwamba Papa Wemba amefariki muda mfupi baada ya kuanguka ghalfa akiwa anatumbuiza wimbo wa tatu jukwaani akiwa na Magic System na kupoteza fahamu, kwenye tamasha aliloalikwa kutumbuiza.
Redio ya Kongo, Radio Okapi imetangaza taarifa za kifo chake kwamba kimetokea nchini humo alikokwenda kutumbuiza kwenye tamasha la muziki la Anoumabo (FEMUA).
Kutoka katika mitandao mbalimbali ya kuaminika duniani, imeelezwa kuwa Papa Wemba aliyefariki akiwa na umri wa miaka 66, alidondoka wiki moja iliyopita na kulazwa hospitalini akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kwa takribani wiki moja kabla ya kufariki usiku wa kuamkia jana.
Chanzo cha kifo cha mkongwe huyo katika muziki wa dansi duniani bado hakijajulikana.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment