
Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, Butusyo Mwambelo
Mbeya. Watu watatu kati ya watano wanaosadikika kuwa ni majambazi wameuawa katika tukio la kurushiana risasi na polisi ambao walikuwa wakijaribu kuzuia uporaji kwenye duka la jumla lililopo Matundasi wilayani Chunya.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa, Butusyo Mwambelo alisema tukio hilo lilitokea jana saa 2:00 usiku katika kijiji cha Matundasi na inadaiwa majambazi hao walitumia pikipiki mbili, moja ikibeba watu watatu na nyingine wawili.
Alisema kuwa polisi walipata taarifa za siri kutoka kwa raia wema na kujipanga kukabiliana nao na kwamba walipofika katika duka la jumla la bia ndipo polisi walipowaona na kuanza kupambana nao.
"Katika mapambanano hayo jambazi mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Baraka, ambaye ni fundi bomba na mkazi wa Makongorosi aliyekuwa na silaha aina ya SMG yenye iliyokuwa na risasi 26 kwenye magazine, aliuawa baada ya kupigwa risasi tumboni na mguuni," alisema.
Butusyo alisema majambazi wengine wanne walifanikiwa kukimbia kuelekea kijiji cha matondo na ndipo askari polisi walipoendesha msakao mkali katika kijiji hicho na baada ya kuwaona polisi waliwashja pikipiki zao kwa nia ya kukimbia huku wakirusha risasi ovyo.
"Ndipo polisi walijibu mapigo na kufanikiwa kuuwa majambazi wengine wawili na kukamata pikipiki moja aina ya Sanlg iliyokuwa ikitumiwa na majambazi hao," alisema.chanzo:mwananchi
0 comments:
Post a Comment