BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKUU WA MKOA WA MBEYA AWABANA MABOSI WA TRA, KISA UBOVU WA BARABARA.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala

Mbarali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala ametoa siku saba kwa uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) mkoani hapa kuhakikisha wanatengeneza maeneo yote korofi kwenye Barabara ya Igurusi hadi Kata ya Utengule - Usangu wilayani hapa.

Makala alitoa amri hiyo jana baada ya kukumbana na vikwazo vya kukwama mara kadhaa katika barabara hiyo kutokana na ubovu wakati akiwa kwenye ziara ya kutembelea wakazi wa kata za Luhanga na Utengule Usangu.

Hiyo ni ziara yake ya kwanza tangu Makala ateuliwe na Rais John Magufuli kuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

“Niseme kuona ni kuamini, sijasimuliwa nimeona mwenyewe, ni barabara ambayo ina kero na inatoa picha halisi kuwa wananchi wanapata tabu ya usafiri wao na wa kusafirisha mazao yao na wagonjwa kutokana na ubovu huu.”

“Natoa siku saba kwa Tanroads wafike haraka kushughulikia maeneo yote korofi pamoja na kuweka makaravati, baada ya siku hizo kwisha, nakuja kukagua tena,” alisema Makala.

Awali, mkazi wa Kijiji cha Luhanga, Maneno Edward alisema wamekuwa wakipata shida kusafiri kwa barabara hiyo kutokana na ubovu hasa kipindi cha mvua za masika.

Alisema mvua zikinyesha barabara hiyo haipitiki jambo linawalowafanya wajawazito kujifungulia njiani na wengine hupoteza maisha. 


“Bora mkuu wa mkoa amekumbana na hali hii ya kukwama, ndiyo inayotoa picha sisi wananchi wa huku tunapata shida kutokana na ubovu huu, hata vyombo vyetu vya moto kila siku vinaharibika kwa ubovu wa barabara hii,” alisema.

Dereva bodaboda, Yasini Kidehile alisema wamepandisha nauli kutoka Sh7,000 kati ya Luhanga hadi Igurusi mjini hadi kufikia Sh 12,000 kutokana na ubovu wa barabara hiyo.

“Unajua mbali na hii adha ya kusukuma pikipiki, kupoteza muda mwingi barabarani, lakini tatizo lingine ni kuharibikiwa kwa vyombo vyetu. 


Hapa kila siku lazima niipeleke pikipiki kwa fundi, hali hii inatufanya tupandishe nauli ili tuweze kuambulia fedha kidogo,” alisema Kidehile. 

Alisema kama Tanroads watatekeleza agizo hilo la mkuu wa mkoa, itawasaidia kuondokana na adha hiyo na gharama za usafiri zitapungua.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: