BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VIPAZA SAUTI VYA UKUMBI WA BUNGE VYASHINDWA KUFANYA KAZI BUNGENI MJINI DODOMA.

Dodoma. Shughuli za Bunge la Muungano leo zilisimama kwa dakika 36 kabla ya kuendelea tena, baada ya vipasa sauti vya ukumbini kushindwa kufanya kazi.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amelazimika kuahirisha shughuli mara baada ya kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu ambacho hata hivyo wabunge walichukua muda mrefu kuuliza maswali kutokana na kuhama hama wakitafuta mahali pa kusikika.

Awali, wabunge waliokuwa na nafasi ya kuuliza maswali kwa siku ya jana walilazimka kuhama maeneo yao na kuzua minong’ono ndani ya ukumbi, huku Mbunge wa Mkuranga (CCM), Abdallah Ulega na Mbunge wa Manonga (CCM), Seif Gulamali wakilazimika kuuliza maswali yao wakiwa uso kwa uso na Waziri Mkuu mbele ya ukumbi.

Hata hivyo, kuna hali ya sintofahamu, kwani vipaza sauti vimeharibika ikiwa ukumbi huo umefanya kazi kwa siku sita tu tangu ulipokabidhiwa baada ya ukarabati mkubwa.

April 18, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alikabidhiwa ukumbi huo ikielezwa kuwa ulikuwa umefanyiwa matengenezo makubwa katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuuboresha.CHANZO:MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: