
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amesema kwenye uzinduzi wa mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za umma kutokana na kuwapo kwa tatizo la watumishi hewa.
“Rais alituagiza kuhakiki watumishi wote na ikafanyika hivyo, lakini kutokana na kuwapo kwa udanganyifu nimeunda timu ambayo imeanza kazi jana (juzi) kuhakiki upya watumishi ili kujiridhisha na kupata ukweli wa watumishi wetu,” amesema.
Makalla amesema timu hiyo imegawanyika katika makundi mawili na kwamba, wajumbe wanatoka idara mbalimbali za Serikali wakiwamo wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment