BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAKUFUNZI WA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA HOMBORO CHAWANOA MADIWANI WA HALMASHAURI ZA KILOSA NA GAIRO KATIKA MAFUNZO ELEKEZI YA SIKU NNE MOROGORO.

Mkuu wa chuo cha serikali za mitaa Homboro mkoani Dodoma, Daktari Emmanuel James Gibai akizungumza jambo wakati akifunga mafunzo ELEKEZI ya uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma kwa madiwani 80 wa wilaya za halmashauri ya Gairi na Kilosa yaliyofanyika kwa siku nne katika hoteli ya Edema Manispaa ya Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG


Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Iddi Mshiri naye akizungumza jambo kwa waheshimiwa madiwani hao hasa kutambua mipaka ya majukumu yao ya kazi na kuzingatia kanuni.
Mwenyekiti wa baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Gairo Morogoro, Rachel Nyangasi akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye hoteli ya Edema Morogoro.
Sehemu ya waheshimiwa madiwani wa halmashauri hizo wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika hafla ya kufunga mafunzo hayo.

Mkuu wa chuo cha serikali za mitaa Homboro mkoani Dodoma, Daktari Emmanuel James Gibai kushoto akizungumza jambo na Mtaalamu wa fedha kutoka mradi wa PS3 mara baada ya mkuu huo kufunga mafunzo hayo ELEKEZI ya uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma kwa madiwani 80 wa wilaya za halmashauri ya Gairi na Kilosa yaliyofanyika kwa siku nne katika hoteli ya Edema Manispaa ya Morogoro.PICHA/MTANDA BLOG
 

Watumishi wa chuo cha serikali za mitaa Homboro mkoani Dodoma wakifuatilia jambo wakati wa kufunga mafunzo ELEKEZI ya uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma kwa madiwani 80 wa wilaya za halmashauri ya Gairi na Kilosa.PICHA/MTANDA BLOG

Saidi


Waandishi wa habari, Lilian Lucas gazeti la Mwananchi, Idda Mushi wa ITV na Anitha Charles kutoka TBC wakiandika dondoo wakati wa hafla hiyo.


Mchungaji wa kanisa la Calvary Assemblies of God kijiji cha Parakwiyo wilaya ya Kilosa na diwani wa kata hiyo, Ibrahim Oloishuro wa pili kutoka kushoto akiwa na waheshimiwa madiwani wenzake wakifuatilia jambo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: