BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MOROGORO YATOA Sh39 MIL KWA VIJANA NA WANAWAKE



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo
 
Morogoro. Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imevipatia vikundi 39 vya wanawake na vijana mikopo ya jumla ya Sh23.8 milioni.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amesema bungeni kuwa vikundi hivyo vyenye wanachama 295 vimepata mikopo hiyo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na Wanawake.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Kusini, Tebweta Omary lililotaka kujua mpango wa Serikali wa kuzibana na kuziamuru halmashauri zote kutenga asilimia 5 ya fedha za mapato kwa ajili ya vijana na asilimia 5 kwa wanawake.

Jafo amesema katika mwaka wa fedha wa 2015/16, Serikali imetenga Sh175 milioni kwa ajili ya kuyawezesha kiuchumi makundi hayo.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: