BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NG'OMBE 603 WATAIFISHWA NA MAHAKAMA YA WILAYA BAADA YA KUINGIZWA KATIKA PORI LA AKIBA BUKOMBE.



Bukombe. Mahakama Wilaya ya Bukombe imetaifisha ng'ombe 603 waliokamatwa wakichungwa ndani ya pori la akiba la Kigosi wilayani humo.

Pamoja na kutaifisha mifugo hiyo, mahakama pia imewahukumu kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh300, 000 kila mmoja watuhumiwa watano waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kuingiza na kuchunga ng'ombe ndani ya pori hilo bila kibali cha Mkurugenzi wa wanyama pori.

Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Bukombe, Gabriel Kurwijila baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa mbele ya mahakama na upande wa mashtaka ulioongozwa na wakili wa serikali Mwasimba Hezron.

HABARI ZAIDI FUATILIA GAZETI LA MWANANCHI LEO.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: