REAL MADRID YAZIBA NGEBE ZA ATLATICO MADRID KATIKA FAINALI YA KOMBE LA UEFA 2016 UWANJA WA SAN SIRO ITALIA.
Usiku wa May 28 2016 Klabu ya Real Madrid imedhihirisha umwamba wake katika michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuilaza Atletico Madrid kaatika mchezo wa fainali na kutwaa ubingwa huo katika uwanja wa San Siro jiji la Milan Italia kwa bao 5-3.
Klabu ya Real Madrid yenye mafanikio katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya wamewaadhibu mahasimu wao Atletico Madrid kwa jumla ya penati 5-3 ushindi walioupata kwa changamoto ya mikwaju ya penaltu baada ya dakika 120 za mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Mchezaji wa Real Madrid, Sergio Ramos dakika ya 15 ndiye aliyeanza kuipatia bao timu yake kabla ya Atletico Madrid kusawazisha kupitia kwa Ferreira Carrasco alilofunga dakika ya 79 na kufanya mchezo huo umalizike bila mbabe.
Ushindi huo unawafanya Klabu ya Real Madrid kuongoza kwa kutwaa Kombe hilo ikiwa ni mara ya 11 huku Atletico Madrid ikishindwa kutwaa kombe hilolicha ya kufika fainali zaidi ya mara mbili.
0 comments:
Post a Comment