BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

USAFIRI WA MABASI YAENDAYO KASI YAWATOA USHAMBA WAKAZI WA DAR ES SALAAM

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakiwa ndani ya basi la Udart katika Kituo cha Magomeni. Mabasi hayo yalianza kutoa huduma kwa majaribio jana na leo kabla ya kuanza rasmi kesho ambako itatoza nauli. Picha na Omar Fungo

Dar es Salaam.
Usafiri wa mabasi yaendayo haraka jana uliwachanganya wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kuchangamkia usafiri wa bure huku wakiibua vituko kutokana na mazoea ya kugombania kupanda, kukaa wawili katika kiti kimoja na kupita njia zisizoruhusiwa.

Waandishi wetu waliokuwa katika vituo mbalimbali kushuhudia majaribio hayo walishuhudia abiria wengi wakishindwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na wahusika ikiwamo wasio na matatizo kuketi kwenye viti vya wenye ulemavu.

Pia, wapo walioonekana wakizunguka na mabasi hayo kutoka kituo kimoja hadi kingine bila kushuka hadi walipoteremshwa kwa nguvu.

Juzi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Udart, Ronald Lwakatare alisema mabasi 140 yangeanza kubeba abiria bure jana na leo katika majaribio.

Baadhi ya maofisa waliokuwa wakitoa elimu juu ya matumizi ya mabasi hayo, walisema kuna changamoto ya wakazi hao kuelewa haraka mfumo wa malipo.

Kwa mujibu wa maelekezo ya maofisa hao, kila abiria atatakiwa kufuata hatua mbalimbali kabla ya kupanda usafiri huo na kushuka.

Hatua hizo ni kulipa na kupewa kadi ambayo ndiyo itakayotumika kuingia na kutoka katika kituo. Abiria wote wanapaswa kutumia mlango wa mbele au nyuma wakati wa kuingia kwa kugusisha kadi hiyo ambayo ndiyo inayofungua mlango.

Baada ya kuingia, basi linapofika kituoni, mlango yake hufunguka sambamba na ilipo ile ya kituoni hivyo kutokuwa rahisi kwa mtu yeyote kupenya. Katika utaratibu huo, ni vigumu kwa abiria kuingia na kutoka bila kulipa kutokana na mfumo huo.

Wakazi wanena
Wakazi wa maeneo ya Ubungo, Kinondoni, Kivukoni, Kimara na Kariakoo waliozungumzia usafiri huo walieleza kuridhishwa kwao na mfumo huo wa malipo licha ya baadhi yao kusema una mzunguko.

Mkazi wa Kigamboni, Mashaka Seif alilalamikia usafiri huo kuchelewa kuanza alfajiri kama ilivyotangazwa, hatua iliyoathiri wengi kufika kwenye maeneo yao ya kazi.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: