BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU DODOMA WAZUA NONGWA BUNGENI KWA NAIBU SPIKA


Dodoma.Naibu Spika wa Bunge ameahirisha Bunge kabla ya muda wake baada ya wabunge kutaka kujadiliwa suala la wanafunzi wa Udom kufukuzwa chuoni wakati hawana kosa.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari aliomba mwongozo na kutaka sakata la wanafunzi hao lijadiliwe lakini Naibu Spika, Tulia Ackson alisema jambo hilo haliwezi kusitisha shughuli za Bunge hivyo haliwezi kujadiliwa kwa wakati huo. 


Kauli hiyo iliwanyanyua wabunge wa upinzani na baadhi ya wa CCM wakipinga kauli hiyo huku wakiwa wamesimama jambo ambalo lilisababisha kuaihirishwa kwa Bunge hadi saa 10:00 jioni huku akiagiza kukutana kwa kamati ya uongozi ya Bunge,MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: