BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAMBO MUHIMU YA KUJUA BAJETI YA MWAKA 2016/2017.


Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango akiwasili bungeni tayari kwa kusoma mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/17 Juni 8 mwaka 2016 huku wabunge wa upinzani watoka nje ya bunge mjini Dodoma.

Kama wewe ni mnywaji wa bia, mvinyo na soda au mvutaji sigara, unamiliki gari, unavaa mitumba au unafanya biashara ya bidhaa kutoka nje, anza kujipanga; maumivu yako mlangoni.

Kuanzia Julai Mosi utalazimika kuvunja ‘kibubu’ kugharimia zaidi bidhaa hizo, kutokana na Serikali kupendekeza kuongeza ushuru wa bidhaa katika bajeti ya mwaka 2016/17 iliyosomwa jana.

Pia, Serikali imependekeza kuanza kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika shughuli za kitalii ikiwamo kuona wanyama na katika ada za huduma za kibenki nchini, isipokuwa kwa riba za mikopo.


Hatua hiyo mpya iwapo itapitishwa na Bunge, itapeleka kilio kwa wananchi wanaotumia huduma za kibenki nchini pamoja na watalii wa ndani na nje.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: