BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA ALIYEKUWA KOCHA MKUU WA NIGERIA.


Kocha Mkuu wa zamani wa Nigeria, Stephen Okechukwu Keshi 
 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa Kocha Mkuu wa zamani wa Nigeria, Stephen Okechukwu Keshi (54) kilichotokea ghafla leo Juni 08, 2016 kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa.

Kutokana na kifo hicho, Rais Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Soka Nigeria (NFF), Amaju Pinnick, familia ya marehemu Keshi pamoja na ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata kuwa nahodha wa kikosi cha Taifa Nigeria ‘Super Eagles’.
 Katika rambirambi ambazo zimefika pia katika Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA), Rais Malinzi amesema kuwa japokuwa Keshi ametangulia mbele za haki, mchango wake kwenye mpira wa miguu hautasahaulika kwani atabaki kuwa alama ya maendeleo ya mchezo wa soka.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: