BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS WA AWAMU YA PILI AWAPIGIA DEBE WANAFUNZI MABASI YA MWENDO KASI DAR ES SALAAM



Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi ameshauri kampuni inayoendesha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Udart), kuongeza mabasi ya wanafunzi na mengine ya wazi juu kwa ajili watalii.

Mzee Mwinyi alitoa ushauri huo jana alipotembelea mradi huo akiwa na mkewe, Sitti Mwinyi na kupokewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wake, Ronald Lwakatare, Mtendaji wa Udart, David Mgwassa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi.

Mwinyi alikata tiketi katika Kituo cha Morocco na kupanda gari kwenda Kariakoo, Gerezani kisha Kivukoni. Mgwassa alisema wananchi wameanza kuelimika, kwani usumbufu na ajali hivi sasa hakuna na kwamba wiki ijayo matumizi ya kadi yataanza baada ya hatua za awali kukamilika.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: