BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI KUWAANIKA WATU, MASHIRIKA WANAOSAMEHEWA KODI.


Waziri wa fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.

Dar.
Serikali kuanza kuwatangaza wanufaika wote wa misamaha ya kodi kila miezi mitatu, ili wadau wafahamu sekta iliyonufaika na maeneo ilikoelekezwa misamaha hiyo.

Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni mjini Dodoma jana, Dk Mpango alisema dhamira ya bajeti hiyo ni kutekeleza ahadi za Rais John Magufuli zilizomo kwenye ilani ya CCM, Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka mitano na Dira ya Taifa ya Maendeleo.

“Utaratibu huu utasaidia kudhibiti wafanyabiashara, taasisi na kampuni zinazotumia vibaya misamaha hiyo kujinufaisha binafsi na watumishi wa umma wasio waadilifu,” alisema Dk Mpango.

Dk Mpango alitangaza marekebisho katika sheria ya kodi ili kuwataka wanufaika kulipa kodi kwa bidhaa watakazoagiza, baadaye kuwasilisha maombi ya kurejeshewa kodi hiyo baada ya uhakiki kufanyika.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: