
wafuasi wa chama cha wananchi cuf.
Pemba. Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria (CUF) Wilaya ya Wete, Mwinyi Juma Ali amesema chama hicho kinaheshimu misingi ya utawala bora na haki za binadamu, hivyo tuhuma za ubaguzi hazina ukweli wowote.
Akizungumza ofisini kwake jana, Mwinyi alisema chama hicho kinasikitishwa na vitendo hivyo hasa kufyekwa mashamba na kusababisha hali ya umaskini kwa wananchi.
Hata hivyo, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman alisema hujuma hizo zinapangwa na kuratibiwa na wafuasi wa CUF.
Othman aliyasema hayo alipozungumza na wananchi baada ya kutembelea shamba la mihogo na migomba, lenye ukubwa wa eka tano lililofyekwa.MWANANCHI

0 comments:
Post a Comment