Mkazi wa kijiji cha Ipera Asilia kata ya Itete Njiwa wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro, Jidaga Lupilimula akiwavusha wakazi wa kijiji hicho katika mto Lwandembo ili kuvuka ng'ambo huku mifugo nayo ikionekana kupiga mbizi katika maji ya mto huo.PICHA ZOTE/MTANDA BLOG
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro, Doroth Mwamsiku akizungumza jambo wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la umoja wa wanawake Tanzania kata ya Sabasaba (UWT) kilichofanyika kwenye ofisi za chama hicho mtaa wa Ngoto mkoani Morogoro, kulia ni diwani wa kata ya Sabasaba, Mudhihiri Shoo.
Mvuvi Jofrey Mwakambaya akiwaanika samaki aina ya kambare baada ya kuwavua katika mabwawa ya maji eneo la Ikotakota kata ya Itete Njiwa wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro kisha kuwauza katika vijiji mbalimbali.
Mfanyabiashara wa kuuza maboga, Luanda Peter akitayarisha mabago katika meza yake kwenye soko la Mawenzi Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kuwauzia wateja wake ambapo boga moja huuzwa kati ya sh1500 hadi sh2000, maboga yamekuwa yakitumika kama futari kwa waumini wa dini ya kiislamu katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani.
Mkazi wa kitongoji cha Kalihanya kijiji cha Ipera Asilia kata Itete Njiwa wilanya ya Malinyi Morogoro, Lenga Lutonjalenga na mkewe Soji Mahongo wakivuna mahindi baada ya kuong'oa mashina ya mahindi hayo na kuhifadhi katika mfumo wa kusimamisha pamoja na hukaa zaidi ya miezi miwili kabla ya kuvunwa.
Mwenyekiti wa chama wa wafugaji Tanzania tawi la Malinyi na Ulanga (CCWT) mkoa wa Morogoro, Michael Pawa, (mwenye fulana nyeupe) akitembezwa moja ya shamba la mahindi linalodaiwa kulimwa eneo lililotengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo katika kijiji cha Ipera Asilia kitongoji cha Ikotakota kata ya Itete Njiwa.
Hatua hiyo imekuja wakati Mwenyekiti huyo akifuatilia mgogoro unaodaiwa baadhi ya wakulima kutoka vijiji vya jirani kuvamia maeneo ya wafugaji na kuendesha shughuli za kilimo.

0 comments:
Post a Comment