
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla ameagiza halmashauri zote mkoa wa Mbeya kukamilisha utengenezaji wa madawati ifikapo JUNI 20 na sambamba na agizo hilo ametaadharisha juu ya takwimu za Madawati Hewa kwa lengo la kuficha ukweli.

Makalla ameyasema hayo leo wilaya ya Mbarali wakati wa ziara ya kukagua utengenezaji wa madawati na hafla ya kukabidhi madawati 162 kwa shule ya msingi Jangurutu.
Mkoa wa Mbeya una upungufu wa madawati 32,000 na mpaka sasa utengenezaji wa madawati umefikia asilimia 95 huku mkuu huyo akitoa hadi tarehe 20 juni kila halmashauri iwe imekamilisha.
Kuhusu udhibiti wa takwimu za madawati hewa ameagiza kila Mkuu wa shule apokee madawati kwa maandishi na yenye ubora kwa idadi Ile ile iliyobainishwa awali kuwa Ndiyo upungufu wa madawati katika Shule zao.
Amewataka wanafunzi na walimu kuyatunza madawati wanayokabidhiwa ili kutoa nafasi kwa serikali, wadau na wananchi kushughulikia changamoto zingine kama ujenzi wa nyumba za walimu,madarasa na vyoo.

0 comments:
Post a Comment