
Shinyanga. Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amesema changamoto nyingi za usafiri wa njia ya barabara zinatokana na watu kutojua sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani.
Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa usalama barabarani juzi, Msovela alisema makosa mengi ya usalama barabarani pia yanasababishwa na watendaji kushindwa kusimamia sheria.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Chacha Maro aliitaka Manispaa hiyo kuhakikisha inakuwa na mpango kazi mzuri kwa ajili ya waendesha baiskeli na wakokota mikokoteni ambao husababisha ajali nyingi barabarani.
0 comments:
Post a Comment