BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KIMBAWALA, MAHARAGANDE WASHINDA UCHAGUZI CHAMA CHA SOKA MANISPAA YA MOROGORO.

Mwenyekiti mpya wa chama cha soka wilaya ya Morogoro (MMFA) Emmanuel Kimbawa kushoto na Katibu Mtendaji wa chama hicho, Kafale Mahalagande wakipongezana mara baada ya kuibuka washindi katika mkutano mkuu wa uchaguzi uliofanyika mkoani hapa.Picha na MTANDA BLOG.

Juma Mtanda,Morogoro
Chama cha soka wilaya ya Morogoro (MMFA) kimepata viongozi wapya baada ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa uchaguzi na kuchagua viongozi mbalimbali wataongoza kwa kipindi cha miaka minne ambao umefanyika julai 24 mwaka huu kwenye ukumbi wa Manispaa mjini hapa.

Akitangaza majina ya wagombea walioshinda katika uchaguzi huo, Mwenyekiti wa kamati huru ya uchaguzi, Omari Mbegu alimtaangaza, Emmanuel Kimbawala kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho baada ya wajumbe kumchagua kwa kumpigia kura za ndio 60 na kura 23 zikimpinga huku kura moja ikiharibika kutokana na kura 84 za wajumbe hao.

Kimbawala ambaye ameshinda nafasi hiyo kiurahisi ilitokana na aliyekuwa mpinzani wake wa karibu, Shomari Kunguge kuenguliwa ikidaiwa kukosa sifa wakati wa kipindi cha uhakiki wa vyeti vya elimu huku Makamu Mwenyekiti, Hashim Saleh naye akipenya katika kiti hicho kwa kupigiwa kura za ndio 74 na kura tisa zikimkataa baada ya kukosa mpinzani.

Kwa upande wa Katibu mkuu mtendaji wa chama hicho, Mbega alimtangaza Kafale Maharagande kuwa Katibu mkuu baada ya kumshinda mpinzani wake, Geofrey Mwatesa kwa kura 45-38.

Wengine walioshinda uchaguzu huo ni pamoja na, Salum Mkolwe
akipitishwa kuwa Mwakilishi wa mkoa kwa kura za ndio 66 wakati kura 14 zikimpinga na nafasi ya Mwakilishi wa vilabu, Ramadhani Wagala akibwagwa kwa tabu na Seleman Masoor kwa kura 42-40.

Mgombea pekee katika nafasi ya Kamati Tendaji, Alex Bulenga aliponea chupuchupu kuangushwa katika nafasi hiyo baada ya kupata kura 40 za ndio huku kura 34 zikimpinga na kura sita wajumbe wakishindwa kupiga kura za ndio au hapana.

“Uchaguzi umemalizika kwa amani na usalama lakini uchaguzi huu umeendeshwa kwa kufuata misingi ya katiba, haki na demokrasia hivyo kamati hii inatoa pongezi kwa walioshinda na jambo la msingi uongozi uliochaguli kuanza mchakato wa kujaza nafasi zilizo wazi ili kukamilisha idadi ya viongozi ndani ya MMFA.”alisema Mbega.

Nafasi zilizowazi baada ya kukosa wagombea ni Mweka Hazina, Mweka Hazina Msaidizi, Mwakilishi Wanawake na upungufu wa nafasi ya Kamati Tendaji huku uchaguzi huo ukikubikwa na mizengwe ya kila aina ikiwemo vilabu zaidi ya 10 wajumbe wake wakizuiliwa kuingia katika ukumbi wa mkutano huo.CHANZO/MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: